MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote nane mkoani Ruvumakutoa kipaumbele cha mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa vikundi vya TASAF vinavyofanya vizuri katika Shughuli za kiuchumi.
Ametoa maagizo hayo wakati anazungumza katika Kikao kazi cha wadau wa TASAF kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kujadili maendeleo ya mpango wa maendeleo ya TASAFkatika wa kipindi cha awamu ya tatu kipindi cha pili.
“Nasisitiza wahusika wote wa utekelezaji wa mpango huu waimarishe uadilifu ,Elimu sahihi kwa walengwa na uwazi katika kutekeleza shuguli zinazohusu upande wa TASAF ili Serikali iweze kufikia malengo yaliyokusudiwa”,alisisitiza RC Ibuge.
Hata hivyo Brigedia Jenerali Ibuge amewapongeza Waratibu wa TASAF kuanzia ngazi ya Taifa,Mkoa na Halmashauri kwa kuwezesha kutekeleza mpango wa kaya maskini ili waweze kuinuka kiuchumi ikiwa utekelezaji wa mpango huu umefanyika katika vijiji na mitaa yote ya Mkoa wa Ruvuma 685 na kaya 67,831..
“Nitumie nafasi hii kuwahimiza viongozi wenzangu wa ngazoi zote washiriki kikamilifu katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za TASAF kwenye maeneo yao ili mpango huu uweze kuwawezesha kaya maskini, watoto na wazee ambao hawajiwezi wapate lishe bora,Elimu na afya “.
Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira amesema Kikao hicho cha wadau wa mradi huo kimeweza kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi kuwa na utekelezaji wa mpango huu katika kipindi cha awamu ya tatu kipindi cha pili.
Mlimira ameyataja mafanikio yaliyotokana na Mradi wa TASAF kwa kaya maskini, kuwa ni wanufaika wameweza kukuza kipato cha kaya kupitia biashara ndogondogo kutokana na fedha ya ruzuku,walengwa 18,044 wamejiunga katika vikundi 1290 vya kuweka akiba na kukuza uchumi mkoani Ruvuma..
Amesema asilimia 99 ya walengwa wanatimiza masharti ya elimu na afya, na jumla ya kaya 19,216 wanaoishi maeneo ya vijijini na mjini wamehamasika kujiunga na mhuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo katika Mkoa wa Ruvuma hadi kufikia Mei mwaka huu kaya zaidi ya 24,000 zimejisajiri katika mfuko wa CHF iliyoboreshwa.
Imeandikwa na Albano Midelo
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma
Mei 14,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.