HIFADHI ya Wanyamapori ya Mbambabay ina jumla ya hekta 597 ikiwa ni milima miwili ambayo ni (Mlima Mbamba wenye hekta 440 na Mlima Tumbi hekta 110 , visiwa viwili vya Lundo chenye ukubwa wa hekta 20 na kisiwa Mbambabay chenye ukubwa wa hekta 27.
Novemba 5, 2022 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Thomas Elias Laban aliwakabidhi rasmi mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) hifadhi hiyo ili waiendeleze kwa kuongeza wanyama na kujenga mabanda ya kupumzikia.
Mpaka sasa jumla ya wanyamapori tisa wamewekwa kwenye kisiwa cha Lundo ambao ni Swalapara watatu na Digidigi sita.
Pamoja na wanyama hao, hifadhi hiyo ina wanyama wa asili kama Pimbi, Tumbiri, Fisimaji, Kenge, Nyoka, Mijusina Ndege wanaishi kandokando ya Ziwa (King fisher, Fish eagle, Commorant, Gunnet, Hammer cock).Mchakato unaendelea wa kuongeza wanyama wengi na kulinda wanyama wa asili na Samaki wa mapambo .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.