• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

IJUE hifadhi ya mistu ya Wino Madaba

Imewekwa kuanzia tarehe: October 8th, 2024

Hifadhi ya msitu wa Wino iliyopo katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma ni miongoni mwa mashamba 24  ya  miti  ya  kupandwa  yanayosimamiwa  na  Wakala  wa  Huduma  za Misitu  Tanzania

Hifadhi  hii  kwa  sasa  ina  ukubwa  wa  hekta  39,718 zinazoundwa na safu tatu (Wino 2,259ha, Ifinga 29,000ha na Mkongotema 8,459ha).

Mhifadhi Mkuu wa Shamba miti Wino Glory Kasmiri anasema uhifadhi ya msitu wa Wino ulianza kuendelezwa na TFS mwaka 2010 ikihusisha eneo dogo la msitu wa asili wenye ukubwa wa hekta 2,259 (ambayo ndio safu ya Wino).

“baadae mwaka 2014 na 2016 tulipata   maeneo   kutoka   vijiji   vya   Mkongotema   na   Ifinga , tangu tumeanza upandaji wa miti mpaka sasa jumla ya hekta 5,495 zimepandwa miti ya jamii mbalimbali lakini sehemu kubwa ikiwa ni misindano’’,anasema Kasimir

Anabainisha kuwa shamba la miti Wino limeendelea kuboresha mahusiano na wananchi,na kwamba katika kutekeleza hayo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia Shamba la miti Wino uliridhia na kufadhili mradi wa maji kijiji cha Ifinga uliogharimu   Zaidi ya milioni 482.

Ametoa rai kwa  wananchi na jamii kutunza mradi huu na maeneo yote ya vyanzo vya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji unakuwa endelevu.

Anayataja malengo makuu ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya msitu wa Wino ni pamoja na:Kuhifadhi maliasili zinazotaka kutoweka na vyanzo vya maji, Vyanzo vya mto upahila – lutukila-luhuhu-Ziwa Nyasa,Mto Mnywa masi – Pitu-Ruhuji-ifakara-Rufiji,Mto  Mwesa – Ruhuji na Mto  Lutukila – Luhuhu.

Mito mingine ni Mgombezi – Lutukila,Mto Kineneka – Lutukila,Mto Kipilili – Pitu,Mto Balali – Pitu,Mto Mapancha – Chechengu-pitu,Mto Mbega – Chechengu na Mto Chechengu – Pitu

Malengo mengine ya kuanzishwa kwa shamba hilo ameyataja kuwa ni kutoa ajira kwa  Watumishi wa kudumu 15, mkataba 10, vibarua wa msimu wanakadiriwa kufikia 4,000,Mazao ya biashara kama mbao na nguzo za umeme kwa siku za usoni ili kuongeza mapato ya serikali n Kuboresha mazingira na hali nzuri ya hewa . Akizungumzia shughuli za upandaji miti katika Shamba la miti Wino,Meneja huyo anasema upandaji miti unaeendelea kufanyika kwa lengo la kuhakikisha uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji vinatunzwa vizuri kwa upatikanaji maji na mazao ya Misitu kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Hata hivyo ameitaja changamoto ya matukio ya moto kwa kiasi kikubwa hupunguza jitihada za usimamizi endelevu wa shamba. Vyanzo vikuu vya moto ni uandaaji wa mashamba msimu wa kilimo kwa kutumia moto ambapo kwa mwaka 2016 ziliungua hekta 600 na 2021 hekta 1,623 ukisababishwa na uaandaaji wa mashamba maeneo ya mabonde yanayopakana na Shamba.

 Katika kukabiliana na tatizo hili, Uongozi wa Shamba la miti wino umekuwa ukitoa elimu na vifaa vya kuzimia moto kwa jamii,kutoa msaada wa vitendea kazi vinavyotumika kuzimia moto kwa jamii,kujenga  mahusiano  mema  na  vijiji  vinavyozunguka  Shamba  kwa kuwapatia vifaa vya ujenzi mbalimbali.

Hatua nyingine zinazochukuliwa amezitaja kuwa ni kufanya kazi za kinga dhidi ya moto (kusafisha Fire lines na kufungua barabara, Kufyekea miti, uwepo wa vituo 3 vya  mawasiliano,  doria  ya  msituni  mwaka  mzima, kuimarisha  ulinzi  wa  kupambana  na  moto  kipindi  chote  cha  kiangazi, kuweka gari standby kwa kiangazi na mfumo wa satelaiti wa kuangalia matukio ya moto uliopo makao makuu ya Wakala.

 

“Shamba la miti Wino linaendelea kuwaomba wananchi kuepuka kuanzisha moto maeneo hatarishi wakati wa uandaaji wa mashamba na kuwataka kufanya maandalizi mazuri ya barabara za kinga moto’’,anasema.

Licha ya changamoto  hizo Shamba  la  Miti  Wino limeweza kufanikiwa kuhifadhi eneo,miti iliopandwa imestawi vizuri,TFS kupitia shamba hili imeimarisha ushirikiano wake na jamii na uongozi katika ngazi mbalimbali,shamba  limetoa  ajira  miaka  yote  kwa  makundi  mbalimbali.  Kwa wastani wananchi 4,000 hujipatia ajira za mda mrefu na mfupi katika shamba hili kwa mwaka.

Anasema shamba hilo pia limevutia wawekezaji wengine kuja eneo hili,kikiwemo Chuo   Kikuu   cha  Sokoine   cha   Kilimo   (SUA)   ambapo   pia wamepewa ardhi na kijiji cha Ifinga.

Anaitaja mipango ya baadaye ya shamba hilo    ni kuhakikisha kwamba mazingira yanatunzwa ipasavyo na upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vya misitu na watumiaji wengine unakua endelevu kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.