UZINDUZI wa Jumuiya ya watumia Maji bonde dogo la Mto Lutukira na Ruhuhu (JUWALURU) na Bonde dogo la Mto Lumecha na Hanga(JUWALUHA) utasaidia kutatua changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya Maji.
Uzinduzi wa Jumuiya hizo umefanyika katika Halmashauri ya Madaba na Namtumbo ambao unatarajia kusaidia vita ya tatu ya Dunia ya ukosefu wa Maji kwa jamii.
Akisoma taarifa Kwaniaba ya Mkurugenzi wa Bonde la Ziwa Nyasa Samwel Yotham amesema Jumuiya zimeundwa kwa Mujibu wa Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 na Sheria ya usimamizi wa Rasilimali za namba 11ya mwaka 2009.
“Lengo ni kuwashirikisha wananchi katika kupanga mpangoshirikishi wa usimamizi wa vyanzo vya Maji,kulinda,kutunza,kuhifadhi”.
Yotham amesema Jumuiya zimejumuisha watumia Maji ambao wamechukua Maji kutoka kwenye vyanzo vya Maji kwa kuweka miundombinu kwenye vyanzo vya Maji kwa matumizi mbalimbali ikiwemo Majumbani,Uanzishaji wa Nishati ya Umeme ,Kamati za umwagiliaji pamoja na ufugaji wa Samaki.
Hata hivyo amesema mchakato wa kuunda Jumuiya umefanyika kwa mujibu wa mwongozo wa uundaji wa Jumuiya za Watumia Maji wa mwaka 2009 na Sheria kwa kufuata taarifa za awali uliofanyika katika vijiji 28.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 27,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.