MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefanya ziara ya kushitukiza katika Kijiji cha Mtupale kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji iliyolenga mapambano dhidi ya corona.
Akizungumza jana na wananchi wa kijiji hicho,kilichopo katika Kata ya Chiwanda Halmashauri ya Nyasa, Mndeme awapongeza wananchi hao namna wanavyopambana na Ugonjwa wa homa ya mapafu ya Corona kwa kuzingatia taratibu zinazoendelea kutolewa na Serikali.
Amewaagiza wananchi uvaaji wa barakoa kwamba wanaweza kujitengenezea kwa gharama nafuu na rahisi kwa kila mwananchi kwa kujishonea ili kupambana na homa ya covid 19.
Hata hivyo Mndeme amewataka Wananchi kuendelea kufanya kazi za kiuchumi na kijamii ili kujipatia kipato katika mahitaji ya kila siku kama alivyoagiza Rais kwamba kila mwananchi achape kazi.
“Sisi Rais wetu kwa mapenzi mema,ameruhusu watanzania tuendelee kufanya kazi ili kupata ridhiki za kila siku,chakula cha kila siku kwa hiyo tufanye kazi wakati huo tukiendelea kuchukua tahadhali.’’,alisema Mndeme.
Mkuu wa Mkoa pia amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa wageni wanaoingia na kutoka katika nchi ya Tanzania ili wawekwe kalantini kwa siku 14 na kwamba wasifikiri kalantini kama ni adhabu bali ni tahadhari itakayosaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini iliyothibitika na Wizara ya Afya kuwa na wagonjwa wa corona.
Imeandikwa na Aneth Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Mei 15,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.