MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Menas Komba amezitaka kamati zinazosimamia miradi katika ngazi ya Kata na Kijiji kushiriki kikamilifu kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
Ameyasema hayo katika kikao cha kutoa mafunzo kwa kamati za ujenzi kwa Kata ambazo zimepokea fedha za kutekeleza miradi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Lundusi-Peramiho.
Pia lengo la kikao ni kuzitambua kamati ambapo wataalamu kutoka Idara ya ujenzi na manunuzi wametoa mafunzo namna ambavyo kamati zinatakiwa kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza Mheshimiwa Komba amewataka wanakamati kujiepusha na vitendo vya hujuma ambavyo vitakwamisha miradi kutokukamilika kwa wakati au utekelezaji wake kuwa chini ya viwango.
Ameongeza kuwa katika ujenzi wa miradi hiyo uzalendo ni kitu cha muhimu hivyo amezitaka kamati za ujenzi kwa kushirikiana na Viongozi wa Kata na Vijiji pale ambapo nguvu za wananchi zinahitajika basi waweze kuwashirikisha na kuwasisitiza ili washiriki kikamilifu.
``Kamati ambazo mnaenda kusimamia ujenzi mkawe makini sana katika kuwasimamia mafundi viongozi hakikisheni kila fundi anaandaa mpango kazi kwani itasaidia sana kujua utendaji kazi wao pia miradi itakwenda kukamilika kwa wakati’’, amesisitiza Mheshimiwa Komba.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Bumi Kasege amewataka mafundi viongozi kushiriki ujenzi kuanzia mwanzo hadi mradi utakapokamilika na sio kuwaachia mafundi wasaidizi ambao wanaweza wasiwe wataalamu na mradi usikamilike kwa viwango vinavyotakiwa.
Vilevile amezisisitiza kamati kununua na kutumia vifaa vyenye viwango vinavyokubaliwa na Serikali na kama ambavyo vimeelekezwa kwenye muongozo wa BOQ.
Nae mtaalamu kutoka ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Bw Patrick Mtavangu amezitaka kamati kutokutengeneza nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya mwajiri kwani ni kosa hivyo amewahasa kuwa waaminifu katika kusimamia miradi hiyo na wasiwe chanzo cha kukwamisha miradi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.