• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

KAMPUNI ya NALIKA Tunduru ilivyodhamiria kuwekeza kwenye utalii

Imewekwa kuanzia tarehe: June 15th, 2022

JITIHADA za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii   kupitia Filamu ya Royal Tour, zimeanza kuzaa matunda baada ya Kampuni ya Nalika Safaris ltd kuamua kuanzisha shughuli zake za utalii katika mji wa Tunduru ukiwa ndio makao makuu ya kampuni hiyo.Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo Frank Laizer alisema, wamekuja wilayani Tunduru kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii wa nchi yetu ndani na nje ya nchi anazozifanya kupitia  Programu ya The Tanzania- Royal Tour.

Alisema,kwa muda mrefu sekta ya utalii imekuwa ikitangazwa sana katika mikoa ya Kaskazini, lakini Nalika Safaris imeona upo umuhimu wa kuwekeza na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mikoa ya kusini  hususani wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Alisema,wamejipanga kuhakikisha kampuni yao iwe moja ya vyanzo vikubwa vya mapato kwa wilaya ya Tunduru na kuwa mlipa kodi na sio kama makampuni mengine ambayo huacha mapato na kodi zake katika mikoa mingine na kuja kuacha sehemu ndogo tu ya mapato yao katika wilaya ya Tunduru.

Kwa Mujibu wake, kuanzishwa  kwa kampuni hiyo wilayani humo,kutasaidia sana kutangaza vivutio vilivyopo Tunduru,na kuchangia mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru  na hivyo kuwa sehemu ya wadau wakubwa wa maendeleo na kutoa ajira za muda na za kudumu kwa baadhi ya Wananchi ambao watapata fedha kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku.


Laizer, amewaomba wakazi wa Tunduru, serikali na wadau wengine kuwapa ushirikiano katika jitihada zao za kutangaza utalii na kufungua fursa mbalimbali kwani Kampuni hiyo ni ya wazawa(Watanzania)kwa asilimia mia moja na ya kwanza kufungua ofisini zake wilayani humo.

Aidha alisema, hatua ya kampuni ya Nalika Safaris kufungua ofisi katika wilaya hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii na kuwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kuwekeza katika sekta ya utalii  katika mikoa ya kusini ambayo kwa muda mrefu imesahaulika.

Laizer amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazozifanya kuitangaza Tanzania Kimataifa kupitia Programu ya Tanzania-The Royal Tour na kuhaidi kwamba, kampuni ya Nalika Safaris itakuwa bega kwa bega  na jitihada hizo kutangaza utalii na kuvutia uwekezaji wa maslahi ya nchi yetu.

Alisema, mpango wao ni kufanya utalii wa aina zote zinazopatikana katika mikoa ya kusini ikiwamo utalii wa  picha, kutembelea maeneo ya Kihistoria, utalii wa uvuvi kwenye mto Ruvuma

ziwa Nyasa na maeneo  maaarufu ya mto Mwambesi pamoja na uwindaji wa kitalii.

Laizer ameiomba Serikali, kufikiria kujenga uwanja wa ndege wilayani humo ili kurahisisha huduma ya usafiri kwa wageni wa ndani na nje ya nchi ambao mara nyingi wamekua wakitamani kufika  wilayani humo lakini wanashindwa kutokana na umbali wa kutoka kwenye viwanja vikuu vya ndege.

Ameeleza kuwa kwa kutumia usafiri wa ndege ni masaa mawili tu kutoka Dar es salaam hadi Tunduru ambapo tayari ni karibu sana na vivutio vingi vilivyopo katika mikoa ya kusini tofauti na sasa ambapo kwa kutumia njia ya barabara ni safari ya siku nzima jambo ambalo kila mtalii anajaribu kulikwepa.

Amewataka wakazi wa Tunduru kujianda kupata mambo mazuri kutokana na uwekezaji wa utalii utakaofanywa na kampuni hiyo ya Nalika Safaris Ltd.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi Wanyamapori ya Nalika Safaris Said Masoud amepongeza jitihada kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kutangaza vivutio vya utalii na kuvutia watu mbalimbali kwa ajili ya

Kuwekeza katika sekta ya utalii hapa nchini.

Akizungumzia kuanzishwa kwa kampuni  ya Wazalendo ya Nalika Safaris alisema, huo ni mwanzo mzuri ndani ya wilaya ya Tunduru na mkoa wa Ruvuma ambao umebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo bado hazijatangazwa vya kutosha.

Alisema, kufunguliwa na kuanzishwa kwa kampuni ya Nalika Safaris wilayani humo kunaonyesha mwanga mkubwa kwa maendeleo katika wilaya ya Tunduru na mikoa ya kusini kwa ujumla ambayo kwa muda mrefu iko nyuma katika masuala ya utalii ukilinganisha na mikoa ya Kaskazini na Pwani.

Ameomba makampuni mengi zaidi kwenda kufungua ofisi zao wilayani Tunduru, ili kuongeza nguvu  kutangaza utalii katika mikoa ya kusini.

Masoud, ameiomba Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii ihakikishe inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyozungukwa na hifadhi za Wanyamapori juu ya umuhimu wa rasilimali zilizopo ili kuepuka migogoro iliyopo kati ya hifadhi na wananchi.

Mkazi wa kijiji cha Rahaleo Asha Ching’amba alisema, hiyo ni fursa kubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo ya Tunduru kuanza kunufaika na rasilimali za misitu na wanyamapori na kuhaidi kutumia nafasi hiyo kujikwamua na umaskini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.