KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Laurian Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Serikali,Wizara,Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanahuisha taarifa mara kwa mara kwenye tovuti za serikali ili ziendane na wakati.
Ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha tatu cha Serikali Mtandao ambacho kinafanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha.
Dkt Ndumbaro amesema tovuti nyingi zina taarifa za zamani na kusisitiza kuwa kuna baadhi ya tovuti zina teknolojia ya mwaka 2012 hivyo ameagiza wahusika wote kubadilisha tovuti hizo ili ziendane na teknolojia mpya.
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kikao hicho alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Jenista Mhagama ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa Deogratias Ndejembi
Kikao hicho kinawashiriki zaidi ya 1200 kutoka mikoa yote nchini,Wizara,Taasisi za serikali na kutoka Zanzibar.
Kikao hicho ambacho kimeanza Februari 8 na kinatarajia kukamilika Februari 10 mwaka huu.
Mamlaka ya Serikali Mtandao mwaka huu inaadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa hapa nchini mwaka 2012.
Ameandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.