Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mary Makondo amewaasa watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na ikiwemo kuwahudumia wananchi ili kufanya utumishi uliotukuka.
Makondo ametoa rai hiyo wakati anazungumza kwa mara ya kwanza na watumishi wa ofisi yake tangu alipoteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea,Makondo amesisitiza kufanya utumishi ulitukuka kwa kuwahudumia wananchi katika ngazi zote,akisisitiza kufanya kazi kwa timu na kwamba ili kufikia malengo ya utekelezaji ni lazima kufanya kazi kwa kufuata sheria,miongozo na kanuni.
“Watumishi ni watekelezaji wa maelekezo ya serikali,ni lazima kuwajibika kwa kufanya kazi kwa bidii,mabalozi wa kwanza ni watu wanaoiona kazi yako,tuishi kwa upendo,umoja na ushirikiano,tuwe hodari katika kuwahudumia wananchi’’,alisisitiza.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo amewakumbusha watumishi hao umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora na kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala anayeshughulikia Rasilimali Watu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Joel Mbewa akizungumza kwa niaba ya watumishi,ameahidi maagizo yote yaliyotolewa na Katibu Tawala kuyatekeleza ikiwemo kufanya kazi kwa bidii na kupunguza malalamiko na kero mbalimbali za wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ina watumishi 110 ambao wanafanya kazi katika Idara nane na vitengo sita.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.