Jumla ya kaya 18,912 zimehitimu mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mkoa wa Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge wakati anazungumza kwenye kikao kazi cha waratibu wa TASAF,wahasibu wa TASAF na maafisa ufuatiliaji wa Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mipango ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.
Amesema hadi kufikia Juni 2024 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na Jumla ya kaya 65,089 za walengwa wa TASAF katika vijiji 685.
Hata hivyo amezitaja kaya ambazo zitaendelea na mpango wa TASAF katika Mkoa wa Ruvuma kuwa ni kaya 46,177.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.