SERIKALI Wilayani Tunduru,imetangaza msako mkali kwa wazazi na walezi wenye watoto ambao wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza kwa muhula wa masomo 2023 lakini hadi sasa bado hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa.
Pia msako huo,utawahusu wazazi na watoto wenye umri na sifa ya kuanza elimu ya awali na msingi na waliokatisha masomo bila sababu za msingi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa watoto wanaodhurura ovyo mitaani.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius,amesema hayo jana wakati akizungumza na Gazeti hili kuhusiana na hali ya mahudhurio kwa wanafunzi waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza na elimu ya msingi mwaka 2023 katika shule mbalimbali wilayani humo.
“Tutawasaka wazazi ambao bado hawajapeleka watoto wao shule ili watueleze kwanini watoto wao wako nyumbani,tutatumia sheria kuwafikisha mahakamani wazazi wasiopeleka watoto wao shule,hii nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria,hivyo ni lazima tutumie sheria zilizopo”alisema Mtatiro.
Alisema wilaya ya Tunduru ni wilaya yenye mwamko mdogo wa elimu,hata hivyo kama viongozi waliopewa dhamana wataendelea kuhamasisha wazazi na jamii umuhimu wa kupeleka watoto shule ili kupata haki yao ya msingi.
Mtatiro ametoa wiki moja kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanapeleka watoto shule na baada ya muda huo kupita serikali haitakuwa na huruma na mzazi au mlezi ambaye atabaki na mtoto wake nyumbani bila sababu za msingi na atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.