OFISI ya Uthibiti ubora wa Shule Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 181 imezinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Lt Josephine Mwambashi.
Akisoma taarifa hiyo katika uzinduzi wa Mbio hizo Mthibiti Mkuu wa Shule Wilaya Tumaini Mbunda amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ni Miongoni mwa Halmashauri 55 zilizopewa fursa ya ujenzi wa Ofisi .
Akielezea lengo la mradi huo kuhakikisha kuwa Serikali inaendelea kuwapatia wananchi wake huduma bora za kielimu zinazokidhi viwango na kuwapatia watumishi mazingira bora ya kufanyia kazi.
Hata hivyo Mbunda amesema mradi umetekelezwa kwa kutumia force account na umesimamiwa na kamati ya ujenzi, ununuzi na ukaguzi pamoja na mapokezi.
Amesema Ujenzi wa jengo hilo ulianza kujengwa Agosti 26,2020 na kukamilika Februari 14,2021 huku zaidi ya shilingi milioni 181 zikitumika katika ujenzi huo.
“Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 wanachi wa Mbinga tunashukuru sana jitihada za Mh.Rais Samia Hassan Suluhu za kuhakikisha huduma za uthibiti ubora wa shule inapewa kipaumbele”
Mbunda amesema miundombinu bora ya kufanyia kazi itasaidia kuongeza ari na ufanisi katika kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mara baada ya kukagua Jengo hilo na kupitia nyaraka ametoa angalizo kwa Mhandishi kuandaa BOQ ili kuacha kuwa wababaishaji katika miradi ya Serikali ambayo inawasidia wananchi kupata huduma kwa wakati sahii.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 4,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.