Waziri wa Afya, Mheshimiwa Jenista Mhagama, amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya na TAMISEMI wamenunua magari ya wagonjwa kwa ajili ya maeneo ambayo hayakuwa na magari ya wagonjwa kikiwemo kituo cha afya cha Mchoteka.
Amebainisha hayo wakati akizindua kampeni kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa katika kata ya Mchoteka wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Mheshimiwa Mhagama ameeleza kuwa wiki mbili zilizopita alikabidhiwa gari la wagonjwa kwa ajili ya kata ya Mchoteka huku akisisitiza si kwa ajili ya Mchoteka pekee bali na maeneo mengine yenye uhitaji wa magari hayo.
“Wiki mbili zilizopita nilikuwa tayari nimeshakabidhiwa gari la wagonjwa la kata ya Mchoteka, sio gari la hapa Mchoteka tu kama kawaida ya Mhe. Rais ni hapa Mchoteka na maeneo mengine yenye shida,” alisema Mhe. Jenista.
Kupitia uzinduzi wa kampeni hizo, Mbunge wa Tunduru Kusini, Mheshimiwa Idd Mpakate, ameeleza kuwa kituo cha afya cha Mchoteka ni cha muda mrefu na kinatoa huduma mbalimbali za afya ikiwemo huduma za upasuaji.
Hata hivyo, amesema kuwa kero kubwa iliyopo katika hospitali hiyo ya kata ni kukosekana kwa gari la kubebea wagonjwa.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali ili kuboresha huduma za afya nchini zikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, utoaji wa vifaa tiba na ununuzi wa magari ya wagonjwa yakisambazwa katika vituo vya afya na hospitali mbalimbali nchini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.