KUELEKEA kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya ameungana na wanawake wilayani humo katika zoezi la upandaji miti katika shule ya sekondari Msindo.
Akizungumza baada ya kupanda miti Malenya ametoa rai kwa wanawake kufanya miradi mbalimbali ya kujiongezea kipato ili waweze kuinua Uchumi wa familia.
Mkuu wa Wilaya amewaasa wanafunzi wanaosoma katika sekondari hiyo,wazingatie zaidi masomo ili waweze kufaulu katika masomo yao ,pia amewatahadharisha kujiepusha na vishawishi kutoka kwa wanaume ili kuepuka kukatisha masomo yao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.