MAKUMBUSHO ya Taifa ya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea,ni miongoni mwa makumbusho saba ya Shirika la Makumbusho ya Taifa na vituo 91 vya kale vilivyopo nchini.
Makumbusho ya Majimaji yalianzishwa na kufunguliwa Julai 6,1980, na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Lawrence Gama,lengo la kuanzisha makumbusho hayo ni kutunza kumbukumbu ya historia ya vita ya Majimaji iliyoanza mwaka 1905 hadi 1907.
Mhifadhi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Adson Ndyanabo anasema Makumbusho hiyo imejengwa katika eneo eneo ambalo mashujaa 67 walizikwa baada ya kunyongwa kikatili na wajerumani.
Analitaja eneo hilo la mashujaa maarufu kama hero square kuna makaburi mawili ya mashujaa moja ni la halaiki ambalo wamezikwa mashujaa 66 katika kaburi moja baada ya kunyongwa na serikali ya wakoloni wa kijerumani Februari 27,1906.
Kwa mujibu wa Mhifadhi huyo,kaburi la pili lililopo kwenye makumbusho hayo ni la Jemedari wa wangoni,Nduna (Sub chief) Songea Mbano aliyenyongwa Machi 2,1906.Mji wa Songea umepewa jina la jemedari huyo.
“Tangu kuanzishwa kwa makumbusho hii usimamizi wake ulikuwa unabadilika mara kwa mara ,kati ya mamlaka ya Mkoa,Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Baraza la Makumbusho ya Majimaji na desturi za Mkoa wa Ruvuma’’,anasisitiza Ndyanabo.
Hata hivyo anasema Desemba 8,2009,Makumbusho ya Majimaji yalikabidhiwa kwa Shirika la Makumbusho ya Taifa la Tanzania,baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuitangaza kuwa Makumbusho ya Taifa kupitia Sheria ya Makumbusho ya Taifa namba saba ya mwaka 1980.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.