• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAAFISA Ugani Ruvuma wapewa mafunzo,wakabidhiwa pikipiki 282

Imewekwa kuanzia tarehe: May 23rd, 2022

MAAFISA Ugani 34 kutoka wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma wamepewa mafunzo ya  maandalizi ya upimaji wa afya ya udongo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Songea Klabu mjini Songea.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa wiki moja kutoka kwa  wataalam wa chuo cha TARI Uyole jijini Mbeya.

Akizungumza wakati  wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Emanuel Kisongo,amesema mafunzo hayo ya wataalam wa kilimo ngazi ya Kata na vijiji yatawajengea uwezo wa kutekeleza zoezi la upimaji wa udongo linalotarajia kufanyika katika vijiji 100 mkoani Ruvuma.

Ametoa rai kwa maafisa kilimo hao mara baada ya kufuzu mafunzo hayo wakasimamie na kutekeleza kwa weledi zoezi la upimaji wa afya ya udongo  katika vijiji ambavyo watapangiwa ambapo kila Afisa Ugani aliyepata mafunzo amepangiwa kufundisha vijiji vinne.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Ruvuma amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pikipiki 282 kwa ajili ya maafisa Ugani wa Kata na vijiji mkoani Ruvuma.

“Maafisa Ugani wa Kata na Vijiji wa Mkoa wa Ruvuma kila mmoja atapata pikipiki moja na seti ya vifaa vya kutolea huduma za ugani katika zoezi la kutambua afya ya udongo katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa’’.alisema Kisongo.

Kwa upande wake Mtafiti Mkuu wa Udongo Kutoka  Chuo cha TARI –Uyole jijini Mbeya Fredrick Mlowe amesema zoezi hili lipo katika awamu ya tatu ya utekelezaji ambapo  awamu ya kwanza ilikuwa mikoa ya Mbeya na Songwe awamu ya pili ilikuwa mikoa ya Rukwa,Mbeya ,Iringa na Morogoro.

Mlowe ameitaja dhima ya mafunzo hayo kuwa ni kwa lengo la kujenga uelewa wa afya ya udongo katika kanda sanjari na  kuzishauri kampuni za uzalishaji wa Mbolea kutoa mapendekezo ya mazao mbalimbali ili yaweze kuzalishwa kwa tija.

Mtafiti huyo amesema matokeo hayo yatawasaidia wazalishaji wa mbolea kutengeneza mbolea inayoendana na hali ya maeneo kulingana na matokeo yaliyopatikana katika upimaji wa afya ya udongo.

Naye Afisa Biashara Mkoa wa Ruvuma Martin Joseph akimwakilisha Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji, amesema maafisa ugani waliopata mafunzo  watasaidia wakulima wa Mkoa wa Ruvuma  kujua matumizi sahihi ya mbolea ili waweze kulima kwa tija.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Mei 23,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.