Maandalizi ya mdahalo kuelekea maadhimisho ya kumbukizi ya mashujaa wa Vita ya Majimaji yanaendelea kwa kasi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
Kikao hicho, kilichoongozwa na Kaimu Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Namtumbo, Ndg. Shaibu Majiwa, kimehusisha pia viongozi wa kimila na desturi wa wilaya hiyo.
Lengo kuu la kikao hicho ni kujadili na kuweka mkakati wa namna bora ya kuendesha mdahalo huo, ambao unatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya maadhimisho ya sherehe za Mashujaa wa Vita ya Majimaji.
Kwa mujibu wa ratiba, maadhimisho ya kumbukizi ya mashujaa wa Vita ya Majimaji kwa mwaka 2025 yanatarajiwa kufanyika tarehe 25 hadi 27 katika ngazi ya mkoa wilayani Namtumbo.
Mdahalo huo unalenga kuelimisha jamii kuhusu historia, madhara, na umuhimu wa Vita vya Majimaji, sambamba na kuwaheshimu mashujaa waliopigania uhuru dhidi ya utawala wa kikoloni wa Kijerumani.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.