MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaomba wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajia kufanyika nchini kote Agosti 23.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake mjini Songea kuhusu maandalizi ya sensa,Kanali Thomas amewaomba wananchi wajitokeze na washiriki kikamilifu zoezi la sensa ya watu na makazi .
RC Thomas ameeleza kuwa mpaka sasa Mkoa wa Ruvuma unajumla ya makarani 5674, ambapo wasimamizi wa maudhuhi ni 571 na wasimamizi wa Tehama 173, ambao watafanya kazi ya kuhesabu watu katika maeneo ambayo wamepangiwa.
Amewataka makarani wa sensa kufanya kazi ya sensa kwa weledi wa hali ya juu, nidhamu kubwa na heshima katika maeneo yao waliyopangiwa
Mkuu wa Mkoa amewaomba wananchi kuandaa taarifa za kaya ili kazi ya kuhesabu watu iwe rahisi na ifanyike kwa muda mfupi,sanjari na kutoa taarifa zinazohusu hali ya ulemavu kwa kuwa wenye ulemavu pia wana haki ya kuhesabiwa.
“Serikali inawaomba wananchi wote kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi kuanzia siku ya Jumanne 23 Agosti 23,2022 kwa kuhakikisha wanashiriki kuhesabiwa na wanahesabiwa mara moja’’,alisisitiza RC Thomas.
Hata hivyo amewatahadhari wananchi kutambua kuwa ni kosa la kisheria kukataa kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi.
Amewahimiza viongozi wa mitaa, Vijiji na Vitongoji kuhakikisha zoezi la sensa katika maeneo yao linafanyika kikamilifu na watu wote wanahesabiwa.
Zoezi la kuhesabu watu linaanza tarehe 23 Agosti, 2022 na linatarajia kuendelea hadi Agosti 28 mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.