KAMPUNI ya Tuteinkwa Investment Company LTD imeanza kuchimba Makaa ya Mawe katika kijiji cha Mtyangimbole Kata ya Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma
Meneja wa Kampuni hiyo Ezekia Makame amesema hadi sasa wamechimba tani 5,000 ambapo mwisho wa mwezi huu Novemba 2023 wanatarajia kusafirisha makaa hayo mara baada ya ukamilishaji wa Barabara inayotoka katika mgodi huo na kufika katika Barabara kuu ya Songea -Njombe.
Hata hivyo Makame amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamaed kwa kutoa ushirikiano katika kampuni hiyo kuanzia utafiti hadi kufikia kuanza uchimbaji wa Makaa ya Mawe.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile ametembelea eneo la mgodi, ambapo ameipongea Kampuni hiyo kwa kuanza zoezi la uchimbaji na upanuzi wa Barabara yenye kilomita 35 ambayo pia itawasaidia wananchi katika shughuli zao za uchumi.
Mkuu wa Wilaya amehaidi kutoa ushirikiano katika utatuzi wa changamoto zilizobaki ikiwemo Barabara na kuhakikisha makaa hayo ya Mawe yanaanza kusafirishwa kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.