Afisa Elimu Awali na msingi katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma Mwl. Saada Chwaya amewapongeza walimu na kuwakabidhi zawadi mbalimbali kwa kuiwezesha Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza Kimkoa katika mitihani ya Taifa ya darasa la saba na darasa la nne mwaka 2023.
Chwaya ametoa Pongezi hizo katika kikao cha tathmini kilichoambatana na sherehe za kuwakabidhi zawada walimu na wanafunzi waliofanya vizuri zilizofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo mjini Madaba.
“Nilijisikia faraja sana katika kikao cha Maafisa Elimu wa Halmashauri 184 wa Nchi nzima na mikoa 26,baada ya Halmashauri yetu kufaulisha kwa wastani wa asilimia 85, Katibu Mkuu wa TAMISEMI alitupatia zawadi ya cheti nikiwemo mimi nawashukuru sana walimu wangu”,alisisitiza.
Afisa Elimu huyo ametoa rai kwa walimu hao kuendeleza wimbi la kufaulisha wanafunzi kwa mwaka huu ili kuendelea kupeperusha bendera ya Mkoa wa Ruvuma kitaaluma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.