HALMASHAURI ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imefanya mafunzo ya utekeleza wa mradi wa BOOST kwa mwaka 2024 /2025.
Katika mafunzo hayo wamehudhuria walimu wakuu sita ambao wamepata mradi watendaji wa vijiji,wahasibu na wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi.
Mratibu wa BOOST katika Halmashauri ya Madaba Raphael Kibirigi amesema wamepokea kiasi cha shilingi milioni 398,800,000/= kwaajili ya ujenzi wa matundu 36 ya vyoo na madarasa 12 katika shule sita za msingi.
Mhandisi wa Halmashauri hiyo Ledemta Lweikiza ametoa rai kwa walimu wote ambao wamepata mradi kuzingatia mwongozo wa ujenzi ,vipimo pamoja na kuzingatia maelekezo yote ambayo watapewa na mhadisi katika ujenzi huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.