• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MADAKTARI bingwa kutoa huduma bobezi kwa gharama nafuu Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 26th, 2025

Wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wamepata neema kubwa ya huduma bora za afya baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kambi ya madaktari bingwa na bingwa bobezi 57 kupitia mpango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Uzinduzi huo umefanyika  katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, ukiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Mary Makondo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Kanali Ahmed Abbas Ahmed.

Bi. Makondo amesema kuwa huduma hizo zitatolewa  kwa gharama nafuu  kwa muda wa siku sita kuanzia Mei 26 hadi 31, 2025, katika hospitali zote za halmashauri ndani ya mkoa wa Ruvuma.

“Kila hospitali ya halmashauri itapokea seti ya madaktari bingwa sita na muuguzi bingwa mmoja,” amesema Makondo. 

“Wataalamu hao watahusisha ubingwa wa magonjwa ya wanawake na ukunga,bingwa bobezi wa magonjwa ya watoto na watoto wachanga,bingwa wa upasuaji na mfumo wa mkojo, bingwa wa usingizi na ganzi, bingwa wa magonjwa ya ndani, bingwa wa kinywa na meno, bingwa wa masikio, pua na koo  na muuguzi bobezi.”

Ameeleza kuwa utekelezaji wa huduma hizo unategemea mazingira bora yaliyowekwa na serikali ikiwemo upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, na miundombinu ya kisasa ya huduma za afya.

Aidha, Bi. Makondo amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuboresha sekta ya afya kwa kasi kubwa, ikijumuisha ujenzi na ukamilishaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, hospitali za halmashauri, vituo vya afya, zahanati na majengo ya huduma za dharura.

Ametoa rai kwa viongozi wa wilaya, halmashauri, wabunge, na madiwani kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa kuhamasisha wananchi kuhudhuria na kunufaika na huduma hizo za kibingwa.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.