• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MADAKTARI Bingwa wa Samia waweka kambi ya siku sita Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 26th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amezindua awamu ya tatu ya kambi ya madaktari bingwa na bingwa bobezi wa Dkt. Samia katika mkoa wa Ruvuma.

Akifungua kambi hiyo ya siku sita itakayoanza tarehe 26 hadi 31 Mei 2025, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Makondo amesema, ujio wa madaktari hao unasogeza huduma karibu zaidi na wananchi hivyo anatarajia kuwa huduma zitakazotolewa zitakuwa kamilifu.

“Serikali yetu imeboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba pamoja na miundombinu ya kutolea huduma za afya, kwa hiyo ni matumaini yangu kuwa huduma zitakazotolewa zitakuwa kamilifu,” alisema Makondo.

Akitoa Salamu za Wizara, Afisa wa Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Bi. Grace Maliki, amesema huduma hizo za madaktari bingwa wa Dkt. Samia zinaletwa karibu na wananchi kwa gharama nafuu ili kuwapunguzia adha ya kufuata huduma hizo mbali na maeneo wanayoishi.

Ametoa wito kwa madaktari hao bingwa na bingwa bobezi kuhakikisha wanawajengea uwezo wataalam wengine ambao watawakuta kwenye maeneo wanayoenda kutoa huduma za kibingwa ikiwa lengo ni kuhakikisha kuwa wataalam hao wanapata ujuzi wa ziada ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi hata baada ya kambi hiyo kumalizika.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dr. Louis Chomboko, amesema moja kati ya mikakati ya serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema ili washiriki kikamilifu katika ustawi wa nchi kwa kuwa wananchi wenye afya ndio wenye tija katika kuzalisha na ustawi wa nchi.

Amebainisha kuwa katika kila hospitali ya halmashauri huduma za kibingwa zitakazotolewa ni za magonjwa ya wanawake na ukunga, watoto na watoto wachanga, upasuaji na mfumo wa mkojo, usingizi na ganzi, magonjwa ya ndani, kinywa na meno wakati huo daktari bingwa wa mifupa atakuwa Songea DC na daktari bingwa wa masikio, pua na koo atakuwa Mbinga TC.

Katibu wa CCM Songea Mjini, James Mgego, akimwakilisha mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, ameeleza kuwa ujio wa madaktari bingwa katika awamu zilizopita umekuwa na mafanikio makubwa katika kutoa huduma za afya kwa wananchi akisisitiza kuwa chama kina imani kwamba hata awamu hii ya tatu italeta matokeo chanya katika kutoa huduma hizo.

Awamu ya pili ya huduma za kibingwa na ubingwa bobezi iliyofanyika kuanzia Oktoba 10 hadi Novemba 03, 2024 katika mkoa wa Ruvuma, wagonjwa 10,819 walihudumiwa na watoa huduma 334 wa fani mbalimali walijengewa uwezo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.