WILAYA ya Songea imefanya Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya (DCC) wakijumuisha Halmashauri tatu Manispaa,Songea,Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini na Halmashauri ya Madaba.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile akizungumza katika kikao hicho amezungumzia uchumi wa madini katika Mkoa wa Ruvuma utakavyochochea uchumi katika wilaya hiyo.
“Ipo haja ya kupata andiko la mchango ,na jinsi uchumi huo utakavyogusa wananchi wengine hasa kwenye sekta ya madini'',alisema Ndile.
Hata hivyo Ndile amezungumzia suala la uchumi wa mazingira ya misitu kutumika katika wilaya ya Songea kwa kuwa Wilaya ya Namtumbo mwaka 2024 wanakaribia kupata Bilioni 4 kupitia misitu kwa kuvuna hewa ukaa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.