Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma limepitisha Mpango na Bajeti ya TSh.bilioni 24.5 kwa ajili kutekeleza shughuli mbalimbali za Halmashauri zilizopangwa kufanyika kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Mpango huo umewasilishwa na Kaimu Afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Regius Sanane katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kepten John Komba , Mjini Mbamba-bay Wilayani hapa.
Bw. Sanane alivitaja vyanzo vya mapato hayo kuwa ni makusanyo ya mapato ya ndani, Matumizi mengineyo, Mishahara(PE) na Miradi ya Maendeleo.
Aliongeza kuwa , bajeti hii inalenga ya kujenga msingi imara na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, kuharakisha maendeleo endelevu, kuboresha hali ya maisha na ustawi wa jamii, na kuharakisha ustawi wa jamii utakaopunguza umaskini haraka.
Aidha,aliyataja malengo mengine ni Kuinua ari ya utendaji kazi wenye tija na ufanisi,kuweka na kuimarisha ushiriki wa wadau wa ndani katika kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali na kutmia uwepo wa mazingira mazuri ya nchi yetu kuimarisha shughuli za biashara kwa lengo la kuifanya Taifa letu kuwa Mhimili wa uzalishaji na kitovu cha biashara.
Maeneo mengine ambayo bajeti imezingatia ni ujenzi wa miundombinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari, kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya, pamoja na kuongeza uzalishaji mazao ya biashara likiwemo,zao la kahawa,korosho na kokoa.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Altho komba ametoa wito kwa wataalam kuendelea na mchakato wa kuiwasilisha bajeti hii sehemu zinazohusika kwa kuwa Baraza la madiwani limeshapitisha ,na Bajeti hii inalenga kutatua Kero za Wananchi wa Wilaya ya Nyasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.