Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kwa kauli moja limepitisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 32.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi. Elizabeth Gumbo, amesema bajeti hiyo itagusa sekta mbalimbali, ikiwemo elimu kwa ujenzi wa mabweni, majengo ya utawala, ukamilishaji wa madarasa, ujenzi wa ofisi za kata, na upimaji wa viwanja.
Ameongeza kuwa bajeti hiyo inalenga kuimarisha vyanzo vya mapato vya ndani pamoja na kulipa madeni ya watumishi na wazabuni.
Madiwani wamepongeza rasimu hiyo na kuiita bajeti ya kimapinduzi, wakisisitiza kuwa itasaidia kutatua changamoto nyingi za wananchi.
Wamemshuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri hiyo.
Baadhi ya madiwani wamesema Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni miongoni mwa halmashauri zinazosimamia miradi kwa ufanisi, wakisisitiza kuwa fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.