• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAHAKIMU wakazi Ruvuma wapata mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa

Imewekwa kuanzia tarehe: October 11th, 2024

Mahakama Kuu Kanda ya Songea  imetoa mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa waheshimiwa mahakimu wakazi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Huntlcub Ruhuwiko mjini Songea,yamefunguliwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mheshimiwa James Karayemaha.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo,Jaji Mheshimiwa Karayemaha amesema Mahakama hiyo iliandaa sera ya mafunzo ya mwaka 2019 kwa lengo la kushusha mafunzo kwenye Kanda hiyo.

Amesema mafunzo hayo yameandaliwa kama sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo ambayo yatawajengea uwezo   waheshimiwa mahakimu kufahamu sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024.

“Mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ,yatawasaidia kujua sheria,kanuni na taratibu zinazoongoza uchaguzi,yatasaidia kujua namna bora ya kupokea ,kusikiliza na kuamua migogoro ya aina yoyote itakayoletwa mbele ya mahakimu’’,alisisitiza.

Hata hivyo ameutaja uchaguzi wa serikali za mitaa ni suala muhimu katika ustawi wa demokrasia nchini ambapo waheshimiwa mahakimu wote  wa Tanzania ni sehemu ya mchakato wa kufanikisha uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ni makamishina wa viapo.

Amewataja waheshimiwa mahakimu kuwa ndiyo  watakaowaapisha wasimamizi wa uchaguzi na viongozi watakaochaguliwa kabla ya kuanza rasmi kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea  amewahimiza watumishi wa Mahakamu kufanya kazi kwa kusikiliza na kutoa maamuzi kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA  hivyo kuachana na matumizi ya karatasi.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo Hakimu Mkazi Mfawidhi,Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Songea Mheshimiwa Japhet Manyama amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa waheshimiwa mahakimu kwa lengo la kuwaandaa kwa ajili ya  kusikiliza na kuamua mashauri yatakayotokea wakati wa  uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amelitaja lengo kuu la mafunzo hayo kuwa ni kuwaandaa na kuwapitisha mahakimu katika sheria zinazohusu uchaguzi zikiwemo kanuni  zinazotumika kwenye uchaguzi wa serikali  za mitaa na kuwaandaa namna ya kumudu msukumo wa kisiasa na jamii kwa kuangalia sheria ili waweze kutoa  maamuzi ya haki kwa wote.

Jaji Mfawidhi wa Mahakamu Kuu Kanda ya Songea Mheshimiwa James Karayemaha akizungumza wakati anafungua mafunzo ya waheshimiwa mahakimu wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Huntclub Ruhuwiko mjini Songea

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.