Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amewataka wananchi wa Songea kulima zao la kahawa ili waweze kujiongezea kipato cha kaya na kukuza uchumi .
Kauli hii ameitoa juzi wakati alipotembelea na kukagua shamba la kisasa la kahawa la kampuni ya Aviv Tanzania lililopo kijiji cha Lipokela wilaya ya Songea
Amesema zao la kahawa lina soko la uhakika nje na ndani ya nchi ambapo linaipatia nchi fedha za kigeni
“Limeni kahawa kama zao la biashara ili mpate fedha za uhakika kutokana na hali ya hewa nzuri na ardhi yenye rutuba ya Songea” alisema Waziri Mkuu
Majaliwa alisema zao la kahawa lina historia nzuri huko nyuma lakini sasa imefutika.Huko nyuma kahawa ilitumika kusomesha watoto lakini hasa kumetokea uzembe na uzalishaji umeshika.
“Nataka maafisa kilimo muwasaidie wakulima kujifunza kilimo bora cha kahawa na kuanzisha mashamba mapya ili wanufaike na zao hili” alisema Majaliwa.
Katika hatua nyingine Meneja Mkuu wa Shamba la AVIV Medu Medappa alisema kampuni yake imezalisha miche milioni mbili ya kahawa lakini hadi sasa ni miche laki mbili tu imechukuliwa na wananchi.
Amewahakikishia wakulima kuwa kuanzia sasa zao la kahawa litanunuliwa kwa njia ya ushirika kupitia AMCOS ili kuwahakikishia na siko la uhakika.
Majaliwa ameonya dhidi ya wataalam wa kilimo wanaotumia muda mwingi kukaa ofisini badala yake watoke na kwenda vijijini kuwaelimisha wakulima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.