• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAJI raslimali adimu Duniani inayohitaji ulinzi -RC Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 2nd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema maji ni raslimali adimu Duniani inayohitaji ulinzi kama zilivyo raslimali nyingine zilizopo kwenye matishio

 Kanali Abbas amesema hayo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.wakati anafunga mafunzo kwa vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya Jamii kwenye mfumo wa kieletroniki wa utoaji ankara za maji na ukusanyaji wa mapato.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku 13 yakishirikisha washiriki zaidi ya 120 kutoka Wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma.

 “Maji ni moja ya matishio makubwa ya kiusalama Duniani,takwimu zilizopo zinaonesha maji yanaendelea kupungua,watu wameyaona maji kama sehemu muhimu ya bidhaa inayohitaji ulinzi,unaofanana na ulinzi wa raslimali nyingine’’,alisema Kanali Abbas.

Hata hivyo amesema baadhi ya maeneo ikiwemo Tanzania haioni tishio hilo kwa sababu kila eneo unalopita unaona maji yanatiririka ambapo amesema maji yanaweza kuiingiza dunia kwenye migogoro ili watu wasiokuwa na maji waweze kuipata raslimali hiyo.

Amesema licha ya uwepo wa maji katika nchi yetu,mapato yanayotokana na uwepo wa maji yamekuwa ni madogo ukilinganisha raslimali nyingine .

Amesema serikali imeamua kuanzisha  mifumo ya udhibiti  wa mapato yanayotokana  na maji ili kudhibiti mapato ya maji na kuhakikisha huduma za maji zinawafikia wananchi kama serikali ilivyodhamiria kuwatua ndoo kichwani.

Amesisitiza kuwa serikali ya Mkoa hivi sasa ipo makini kubaini matumizi mabaya ya fedha ambazo zitakuwa zinakusanywa kutokana na  raslimali ya maji.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge amewaasa washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha maji yanafika kwenye nyumba za wananchi na fedha inayokusanywa inapelekwa benki.

Amesema kwa kuwa fedha hizo zinakusanywa kupitia mfumo inamaanisha fedha hizo ni za serikali ambazo zina utaratibu wake maalum wa matumizi na kwamba kwenda kinyume  na hivyo ni kujitafutia matatizo.

Katibu Tawala huyo amewaomba washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha kuwa fedha itoke kwa utaratibu maalum na kutumika inavyostahili ili kufikia malengo yaliyowekwa badala ya kutumia fedha mbichi.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga amelitaja lengo mafunzo hayo ni kuhakikisha RUWASA inatekeleza maagizo ya serikali ya kukusanya fedha za serikali kupitia vyombo vya watumiaji maji na kutumika kwa malengo ya serikali.

Lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.