Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema makaa ya Mawe ya mawe yanayochimbwa kwenye mgodi wa Ngaka wilayani Mbinga wakati wowote kuanzia sasa yataanza kuuzwa nchini India.
Akizungumza na wananchi wa Mbinga,Mndeme amesema makaa ya Mawe hayo ambayo utafiti umebaini yanaongoza kwa ubora duniani, yataenda kuendesha viwanda vilivyopo ndani na nje ya Nchi kutoka.
Amesema madini hayo ni kichocheo cha ukuaji wa Uchumi katika Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla ambapo, ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Mbinga kuendelea kuwekamazingira rafiki kwa wawekezaji ili waweze kuwekeza katika sekta hiyo ya madini katika kukuza uchumi.
‘’Tayari Rais wetu amekwisha kutuletea Meli za mizigo katika ziwa Nyasa na hizo Meli zimeanza kufanya kazi tayari zimeanza kubeba Makaa ya Mawe kupeleka ndani ya nchi na nchi zingine’’,alisema Mndeme.
Hata hivyo Mkuu wa koa ametoa rai ya kwa kampuni za madini kuchimba makaa ya mawe kwa wingi katika mkoa wa Ruvuma kwasababu njia za usafirishaji ni rafiki hivyo kasi ya uchimbaji iongezeke zaidi ili kupata mapato mengi zaidi.
Mkuu wa Mkoa amewataka wachimbaji kuchimba usiku na mchana ili makaa ya Mawe yaweze kutumika kama nishati katika viwanda vyetu vya ndani na nje ya Nchi na ni chanzo cha Mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Utafiti uliofanywa mwaka 2008 unaonesha kuwa makaa ya mawe ya Ngaka yanaongoza kwa ubora Duniani.Katika eneo hilo zimegundulika tani milioni 400 za makaa ya mawe ambazo zinatarajiwa kuchimbwa kwa miaka zaidi ya 100.
IMEANDIKWA NA ANET NDONDE
OFISI YA HABARI YA MKOA WA RUVUMA
JUNI 2,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.