MKOA wa Ruvuma una vivutio vingi tofauti ambavyo bado havitumiki katika kuchangia pato la Taifa na kuinua uchumi wa wananchi wa eneo husika.
Jiwe la Mbuji ambalo lipo katika wilaya ya Mbinga ni miongoni mwa vivutio adimu na vya kipekee vilivyopo katika Bonde la ziwa Nyasa ambalo linajumuisha mikoa ya Mbeya,Ruvuma na Njombe.
Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Africanus Challe anasema tayari Idara yake imeliingiza jiwe la Mbuji kwenye orodha ya vivutio vya utalii katika Mkoa wa Ruvuma ili hatimaye kazi ya kutangaza eneo hilo na vivutio vingine iweze kufanyika kwa tija.
Kivutio cha jiwe la Mbuji kimekuwa gumzo kwa wengi waliosikia taarifa za kivutio hicho.Neno Mbuji kwa lugha ya kabila la wamatengo ni "Kitu kikubwa",jiwe hili lipo katika kijiji cha Mbuji kata ya Mbujii na limekuwa kivutio adimu kwa wageni wa ndani na nje ya nchi.
Jiwe la Mbuji lina maajabu mengi yakiwemo jiwe pekee kubwa Mkoani Ruvuma,lina vyanzo vingi vya maji chini yake,ni vigumu kulipanda bila kuwaona wazee kwa sababu ni vigumu kupanda na kulizunguka jiwe hilo bila kufuata mila na desturi za kabila la wazee wa kimatengo.
Unapofika katika jiwe hilo inakulazimu kuwatafuta wazee wanaotoa maelekezo kwa yeyote anayetaka kupanda jiwe hilo,ambalo linaheshimika sana na wakazi wanaolizunguka jiwe hilo.
Ili kupanda jiwe hilo ni lazima uwe na Mwongozaji ambaye ni mzee wa mila ambaye anazifahamu vizuri mila na taratibu za kabila la wamatengo zitakazokuwezesha kupanda jiwe hilo bila matatizo na kufurahia vivutio vilivyopo.
Historia inaonesha kuwa jiwe ka mbuji tangu zamani lilikuwa linatumiwa na wazee kwa ajili ya kutambika katika mila na desturi kwa kufuata mila na desturi ikiwemo kutumia unga wa mhogo na kujipaka kabla ya kuanza kupanda jiwe hilo.
“Iwapo mtalii ataamua kupanda jiwe hilo bila kuwaona wazee wa mila na desturi atakuwa amevunja mila na desturi na anastahili kupata adhabu na hata kushindwa kulizunguka jiwe hilo”, anasisitiza Ndunguru.
Ili kulimaliza jiwe hilo kulizunguka inachukua kati ya saa 12 hadi 14 ingawa muonekana wake kwa macho unaweza kulimaliza kulizunguka jiwe hilo hata kwa nusu saa tu.
Jiwe la Mbuji pia hutumika kuwaombea watu wanaosumbuliwa na mapepo ambao hupandishwa juu ya jiwe hilo na kuombewa kimila na kwamba inaaminika mapepo hayo huondoka na wagonjwa wa mapepo wanakuwa wamepona kabisa wanaposhuka chini ya jiwe hilo.
Kutokana na maajabu hayo Ndunguru anasema ndiyo maana jiwe hilo linaitwa jiwe la maajabu ambayo yanavutia wengi.
Uchunguzi umebaini kuwa unapoliangalia jiwe la mbuji kwa mbali linaonekana kwamba ni fupi lakini kadri unavyolikaribia ndivyo jiwe hilo linavyoonekana kuwa refu na kuwa na ugumu kulizunguka lote kwa muda mfupi hali ambayo inasababisha watalii wengi wanaotembelea jiwe hilo kuona hayo ni maajabu ambayo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.