• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAKAMU wa Raia kuzindua maonesho ya nanenane,Mkoa wa Ruvuma kuonesha fursa za kilimo na ufugaji

Imewekwa kuanzia tarehe: August 1st, 2023

I

Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, anatarajia kuzindua rasmi maonesho ya NaneNane tarehe 01.08.2023  ambapo Kitaifa yatafanyikia Jijini Mbeya katika Viwanja vya Nanenane vya John Mwakangale, kama zilivyo fursa nyingine hii pia ni moja ya fursa adhimu kwa wakulima na wafugaji kujifunza namna ya kufuga na kulima kisasa, kwa kutumia fursa mbali mbali zinazotolewa na Serikali, ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA”

Kama ilivyo kwa Halmashauri nyingine katika mikoa ya Tanzania, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, nayo ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zitatoa huduma kwa wakulima, wafugaji na wananchi wengine, kwa siku kumi mfululizo kwanzia tarehe 1/08/2023 mpaka tarehe 10/08/2023, ambapo kwa upande wa Nyanda za juu kusini, itafanyika Jijini Mbeya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndg. Neema M. Maghembe, anawakaribisha wananchi wote kwenye maonesho hayo, kwa ajili ya kupata Elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wetu, ambao kupitia fursa hiyo wanaweza kujiajiri na kuongeza kipato kwao, familia zao na Taifa kwa ujumla.

Pamoja na hayo, mtaalam mwenye dhamana ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Songea Ndg. Hellen Shemzigwa, pia ametoa wito kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali, kwenda kujifunza namna na njia rahisi ya kulima mazao ya kibiashara, na namna ya kufuga mifugo tofauti, tofauti kwa kutumia mbinu rahisi na za kisasa.

Miongoni mwa mifugo ambayo, Halmashauri ya Wilaya ya Songea itatoa elimu, ni pamoja na ufugaji wa Samaki, ufugaji wa ng’ombe wa kisasa, ufugaji wa kuku, bata na ufugaji wa nyuki.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.