Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango Disemba Mosi, 2024 amekabidhi magari aina ya Lori 28, Double-Cabing 68 yenye vifaa vya baridi pamoja na pikipiki 300 zenye thamani ya Shilingi Bilioni Nane ambayo yatasambaza huduma za chanjo kote nchini.
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amekabidhi magari hayo wakati wa kilele cha siku ya UKIMWI Duniani na anatarajwa kuhitimishwa leo kwani maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ifikapo Disemba mosi na kwa mwaka huu yamefanyika kitaifa mkoani Ruvuma.
Baada ya makabidhiano hayo Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema magari hayo yatapelekwa katika mikoa minne ambayo ni Mkoa wa Ruvuma, Njombe, Lindi pamoja na Mkoa wa Mtwara na baada ya kukabidhi Wizara ya Afya itasimamia magari mengine ili yaweze kufika nchi nzima.
"Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, magari haya pia yatapelekwa upande wa pili wa muungano - Zanzibar ili kuhakikisha tunadhibiti magonjwa yanayoweza kudhibitiwa kwa chanjo ambayo yanakuwa ni mafanikio kwa pande zote mbili," amesema Waziri Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama amesema magari hayo yatasaidia kuwafikia na kuwalinda watoto wote dhidi ya magonjwa hatarishi ambayo yanaweza kuepukika kwa kutekeleza vizuri huduma za chanjo ikiwemo chanjo ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike.
Waziri Mhagama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mahiri wa kidiplomasia kwa kuunganisha mataifa ambayo yamekuwa yakiisaidia Tanzania hasa katika Sekta ya Afya.
"Mhe. Mgeni rasmi, tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na dhamira yake nzuri ya uongozi wa kidiplomasia ya kuendelea kuleta maendeleo katika Taifa hili ikiwemo hapa nkoa wa Ruvuma na kwenye Sekta ya Afya kwa lengo la kuendelea kuhudumia wananchi," amesema Waziri Mhagama.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.