Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua magari 96 pamoja na pikipiki 300 zilizotolewa na shirika la kimataifa linalojishughulisha na upatikanaji wa chanjo (GAVI) kwa ajili ya usambazaji wa chanjo nchini.
Uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani hapo.
Makamu wa Rais amesema magari na pikipiki hizo zenye thamani ya shilingi Bilioni 8 zilizotolewa kwa ajili ya kuimarisha huduma za chanjo katika Halmashauri zitasaidia kuboresha huduma za chanjo na kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa yanayozuilika.
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amesema magari na pikipiki hizo zitatumika katika usambazaji wa chanjo nchini ili kuhakikisha magonjwa yanayoweza kudhibitiwa kwa watoto yanadhibitiwa.
Amesema magari hayo yatakabidhiwa kwa mikoa minne ya karibu ukiwemo Mkoa wa Ruvuma, Njombe, Lindi na Mtwara na baada ya hapo Wizara ya Afya itasimamia ufikishwaji wa magari hayo katika mikoa mingine ya Tanzania na Zanzibar.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.