KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Komred Oddo Mwisho imekagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi mchepuo wa kiingereza inayoitwa Chief Zulu Academy inayojengwa Mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano Manispaa ya Songea.
Mradi unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 500 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Mradi umefikia asilimia 60 na shule inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi Januari 2024
Kamati imeridhishwa na ubunifu wa mradi huo na kutoa rai kwa Halmashauri nyingine za Mkoa wa Ruvuma kubuni miradi mipya yenye tija
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.