Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameongoza kikao kazi cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya kata kwa kipindi cha Aprili – Juni 2021, kilichofanyika leo tarehe 02 Julai 2021 katika ukumbi wa Manispaa Songea.
Pololet amesema tathimini hiyo imefanyika kwa lengo la kuhakiki utekelezaji wa mkataba wa lishe kutoka kata 21 ndani ya Manispaa ya Songea, ambazo zinaonesha idadi halisi ya watoto wenye utapiamlo ambapo kwa sasa utapiamlo umepungua kwa kiwango cha asilimia 100% ukilinganisha na kipindi cha robo mwaka Januari- Machi 2021 ambapo takwimu zinaonesha idadi ya watoto wenye utapiamlo ilikuwa ni asilimia 0.6%.
Amewataka maafisa watendaji wa kata, maafisa watendaji wa mitaa na wahudumu wa afya kuendelea kutembelea kwenye kaya za wa mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili kuwapatia elimu ikiwemo na kuhakikisha wanahudhuria kliniki mara kwa mara.
Naye Afisa lishe Manispaa ya Songea Frolentine Kissaka amesema miongoni mwa changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa lishe kwa jamii ni pamoja na kuwepo kwa kiwango kidogo cha utambuzi wa watoto wenye utapiamlo hususani ( utapiamlo mkali katika jamii), na baadhi ya kata kuchelewa kuleta taarifa zinazohusiana na tekelezaji wa mkataba wa lishe katika mitaa yao kwa wakati.
Pamoja na changamoto hizo Halmashauri Manispaa ya Songea imefanikiwa katika utekelezaji wa lishe ya jamii katika kipindi cha aprili hadi juni 2021 kwa kupungua utapiamlo kwa asilimia 100% , hii ni kutokana ushirikiano na ukaribu wa jamii pamoja na mwitiko mkubwa wa viongozi ngazi ya Wilaya, Halmashauri, kata na Mitaa.
Alisema Mikakati ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika kutekeleza Mkataba wa Lishe kwa jamii ni pamoja na kuwawezesha wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kuimarisha usimamizi kwenye mitaa/ kata ambako ni sehemu kubwa ya kiini cha kuleta mabadiliko katika jamii ili kuongeza wigo wa kufanya kazi za uchunguzi wa hali ya lishe na kuweza kuibua watoto wengi wenye tatizo la utapiamlo ngazi ya mitaa. ‘Kissaka alieleza’.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.