• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MAZAO ya biashara yaleta mapinduzi Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 29th, 2025

Uzalishaji wa mazao ya biashara katika Mkoa wa Ruvuma umefikia hatua ya juu ya kihistoria, baada ya zao la tumbaku kufikia tani 2,053 kwa msimu wa 2024/2025, kutoka tani 1,664 msimu uliopita.

Ongezeko hilo limeashiria kurudi kwa nguvu kwa wakulima katika sekta ya kilimo cha biashara, huku wakinufaika na mifumo rafiki ya masoko na ongezeko la bei katika soko la dunia.

Kwa upande wa zao la ufuta, hali ni ya matumaini makubwa zaidi baada ya kufikia tani 5,538 katika msimu huu, huku matarajio yakiwa ni kuvuna hadi tani 10,000 msimu ujao wa 2025/2026.

Ongezeko hilo limechochewa na utekelezaji madhubuti wa mfumo wa stakabadhi ghalani na juhudi za vyama vya ushirika kuratibu masoko kwa ufanisi.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Mazao Songea Namtumbo (SONAMCU) uliofanyika  mjini Songea, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Mary Makondo, amesema mafanikio hayo yanadhihirisha mchango mkubwa wa ushirika katika kuinua kipato cha wakulima na uchumi wa mkoa.

Ameipongeza SONAMCU kwa kuwa nguzo muhimu katika uendeshaji wa masoko ya mazao na kuwahakikishia wakulima maslahi yao.

Katika hatua nyingine muhimu, Makondo ametangaza kuwa msimu mpya wa minada ya ufuta utaanza rasmi  Mei 29, 2025 katika Wilaya ya Namtumbo, akiwataka wakulima kujitokeza kwa wingi ili kufaidika na bei nzuri zinazopatikana kupitia mfumo rasmi wa minada unaolenga kuwapatia tija kubwa zaidi.

Kwa upande wake, Meneja wa SONAMCU, Juma Mwanga, ameeleza kuwa chama hicho kimejipanga kikamilifu kuratibu masoko ya mazao ya biashara kama tumbaku, mbaazi na ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, ambao umeongeza uwazi, usalama wa mauzo, na mapato kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma.

Kuimarika kwa uzalishaji wa mazao ya biashara mkoani Ruvuma ni ushahidi wa mafanikio ya sera za ushirika na mifumo ya kisasa ya masoko.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.