• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MBAMBABAY wapongeza barabara za lamı za mitaa

Imewekwa kuanzia tarehe: January 21st, 2025

BAADHI ya wakazi wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma,wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Barabara za vijijini na mijini(TARURA) kwa kuboresha miundombinu na kujenga  barabara za mitaa katika mji mdogo wa Mbambabay kwa kiwango cha lami.

Wamesema,ujenzi wa Barabara hizo umesaidia kurahisisha huduma ya usafiri  kutoka sehemu moja  kwenda nyingine, kuondoa adha ya vumbi kipindi cha kiangazi na matope kila inapofika msimu wa mvua pamoja na maeneo yao kupanda thamani ikilinganishwa na siku za nyuma.

Petro Zambala mkazi wa Mbambabay alisema,uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita kujenga barabara kwa kiwango cha lami katika mji huo utaharakisha maendeleo  na kuchochea kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na wilaya ya Nyasa.

Alisema,kabla ya barabara za lami baadhi ya huduma za kijamii zilipatikana kwa shida  kwa sababu walishindwa kufika maeneo ya kutolea huduma hizo kwa wakati, jambo lililosababisha kuwa na maisha magumu.

Mkazi mwingine wa Mbambabay Nikaya Mbalale alisema,tangu Serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani  kuna mabadiliko makubwa katika mji huo hasa baada ya TARURA kupatiwa fedha nyingi ambazo zimewezesha kuboresha miundombinu ya barabara zake kwa lami, tofauti na siku za nyuma ambapo barabara nyingi za mitaa zilikuwa za vumbi.

Alisema,kuimarisha na kuboreshwa kwa barabara hizo zimehamasisha na kuwavutia watu wengi kwenda kuwekeza katika Mji wa Mbambabay  ambao wananchi wake wanategemea shughuli za uvuvi na kilimo ili kuendesha maisha yao.

“ni jambo la faraja  kwetu sisi wananchi Serikali yetu ya awamu ya sita kutujengea barabara za lami kwenye mitaa yetu,siku za nyuma tulipata shida kubwa kupitia kwenye maeneo haya kwenda kutafuta huduma za kijamii kwenye maeneo mengine”alisema Mbalale.

Aidha Mbalale,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha kukamilisha ujenzi wa mradi wa barabara ya Mbambabay- Mbinga yenye urefu wa kilometa 66 kwa kiwango cha lami.

Alisema,kukamilika kwa barabara hiyo kumesaidia kupunguza gharama za maisha na usafiri kwani  hapo awali  walikuwa wanalipa  Sh.15,000 nauli ya kutoka Mbambabay hadi Mbinga lakini  kwa sasa wanalipa Sh.9,000 hadi 10,000.

“kabla ya barabara ya lami ya Mbambabay-Mbinga,wilaya yetu ya Nyasa ilikuwa kama kisiwa kila inapofika msimu wa masika,barabara zilijifunga hivyo kuathiri shughuli za usafiri na usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali”alisema.

Alisema,Rais Samia Suluhu Hassan  na Serikali yake imemaliza kero hiyo,sasa magari yanafika na kuondoka kwenye mji wa Mbambabay muda wowote na wananchi wanafanya shughuli zao za uzalishaji mali.

“awali kila inapofika kipindi cha masika tulikuwa kwenye mateso makubwa sana kwani barabara zote zilijifunga kutokana na ubovu wa barabara,magari pekee yaliyoweza kufika katika wilaya ya Nyasa ni LandRover tu,hali hii ilipelekea tuwe na maisha magumu sana”alisema Mbalale.

Jackob Madondola alisema,miaka ya nyuma kila inapofika msimu wa masika  wananchi wa Mji wa Mbambabay walikuwa kwenye mateso makubwa kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kutiririsha maji kwenda Ziwa Nyasa.

Alisema,tangu TARURA ilipoboresha miundombinu kwa kujenga barabara za lami na mifereji ya kupitisha maji wananchi wanaishi kwa amani na wanapata muda wa kufanya shughuli za kuwaingizia kipato bila hofu badala ya kubaki nyumbani pindi mvua zinaponyesha ili kuokoa mali zao zisisombwe na maji.

Alitolea mfano katika mlango wa kuingia kituo cha afya Mbambambay, kulikuwa na miundombinu mibovu ya barabara  iliyokwamisha kuwahisha wagonjwa  hasa akina mama wajawazito na watoto kupata huduma za haraka ili kuokoa maisha yao.

“kwa hiyo uletaji wa fedha katika wilaya yetu umesaidia sana kumaliza kero ya usafiri na usafirishaji kwa kiwango kikubwa na sasa wananchi wanaishi vizuri na kwa amani wakati wote,tunaishukuru Serikali kupitia TARURA kwa kazi nzuri iliyofanya”alisema.

Kaimu meneja wa TARURA Wilaya ya Nyasa Derick Theonest alisema,TARURA inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kwa kujenga barabara za lami  ili kuboresha mazingira na maisha ya wananchi wa mji wa utalii wa Mbambabay na wilaya ya Nyasa kwa ujumla.

Alisema,hadi sasa wamebakisha kilometa1  ili kukamilisha barabara za lami katika mji wote wa Mbambabay na kuishukuru Serikali kwa kuendelea kuipatia TARURA fedha  kwa kujenga miundombinu ikiwemo barabara za lami ambazo zina mchango mkubwa katika kuchochea na kuharakisha maendeleo.

Amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza na kulinda miundombinu ya barabara hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu kwani zinatumia fedha nyingi kuzitekeleza.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.