• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MBATI kijiji pekee duniani kilichopo mkoani Ruvuma chenye miti iliyogeuka mawe,inayovutia wengi

Imewekwa kuanzia tarehe: December 7th, 2020

Kijiji cha Mbati kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kimebarikiwa kuwa na msitu wenye magogo yaliyogeuka mawe hali inayosababisha kutembelewa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Mratibu wa Utalii Kanda ya Kusini ambaye pia ni Afisa Msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Tunduru Debora Mwakanosya  amesema miti inayogeuka mawe (Miti mawe) ni jamii ya miti ya mitetereka ambayo duniani inapatikana nchi mbili ambazo ni Marekani na Tanzania.

“Kwa Tanzania miti mawe inapatikana Mkoa wa Ruvuma  katika kijiji cha Mbati wilaya ya Tunduru,pia miti hiyo inapatikana katika Wilaya ya Namtumbo eneo la Likuyu Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na katika pori la Akiba la Liparamba wilaya ya Nyasa’’,alisema.

Amesema mti huo ukiuona juu kabla ya kugeuka jiwe unakuwa ni mti wa kawaida na kwamba mti huo unageuka jiwe kutokana na mfumo wa asili ambao Mungu ameutengeneza kwa kuwa mti huo unageuka jiwe zito kabisa.

Amesema kivutio hicho cha miti mawe kinaufanya utalii wa Mkoa wa Ruvuma kuwa ni wa kipekee na tofauti kabisa na kwamba aina hiyo ya miti ina uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 120.

Hata hivyo Mtaalamu huyo wa miti amesema miti hiyo ipo katika hatari kubwa ya kutoweka kutokana  na watu wengi kuikata kwa matumizi mbalimbali,ambapo amesisitiza miti hiyo inatakiwa kuhifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Naye Sandali  Mtenje Mzee maarufu katika kijiji cha Mbati chenye  msitu wenye magogo yaliyogeuka mawe,amesema aliona vipande vya mti uliogeuka mawe tangu mwaka 1983 na kwamba miaka hiyo vipande hivyo vya magogo vilikuwa katika hatua za awali za kugeuka mawe.

Sandali anasema miaka tisini waliona wageni wengi wanatembelea mara kwa mara msitu wa kijiji hicho wakiwemo raia wa kigeni ambao walifika kuona miti hiyo ikiwa imegeuka mawe.

“Baada ya muda tukagundua wazungu wanafika hapa tena bila hata kuona viongozi wa kijiji wanapandua magamba ya miti hiyo na wengine wanachukua vipande vya miti iliyogeuka mawe na kuondoka navyo’’,alisema Sandali.

Utafiti uliofanywa katika pori la akiba Selous ambalo sasa ni hifadhi ya Taifa ya Nyerere  na wataalam kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Maliasili na Utalii umebaini kupatikana zaidi ya aina(species) 2100 za mimea zilizotambuliwa na wanasayansi ikiwemo aina 600 za miti ambayo haipatikani sehemu nyingine duniani.

Mkurugenzi Mstaafu wa Uhifadhi ambaye pia amewahi kuwa Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori Likuyuseka Namtumbo  Ngwatura Ndunguru anaitaja Moja ya  jamii ya miti ambayo haijafahamika na kutangazwa ipasavyo  kuwa ni  magogo ya miti iliyogeuka mawe jamii ya miti ya mitetereka ambayo kitaalam inaitwa fossilized tree trucks .

Amesema masalio ya magogo  hayo  bado yanaonekana katika baadhi ya maeneo ya ndani hifadhi ya Selous(Hifadhi ya Taifa ya Nyerere) na  katika vijiji vya Mpurakacheche na Mbarang’andu Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.

Ngwatura anasisitiza kuwa miti mawe hiyo ikitangazwa kwenye vyombo vya habari,mamia ya watalii wanaweza  kufika katika Mkoa wa Ruvuma na kuona kivutio hicho kipya na cha kipekee  hivyo  kuingiza mapato na fedha za kigeni ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Afisa Utalii wa Pori la akiba Liparamba wilayani Nyasa Maajabu  Mbogo amesema miti mawe inapatikana kwa wingi katika eneo la Nakatuta ndani ya hifadhi hiyo.

Kwa mujibu wa Mhifadhi huyo,maeneo yote ambayo miti imegeuka mawe hayakaliwi na watu wengi wala hakuna mtu anayeingia ndani ya eneo hilo hali iliyosababisha maeneo hayo kubakia katika hali yake ya asili ya kijiolojia ya kutoharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Desemba 7,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.