Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma wametakiwa kushiriki ipasavyo katika utekelezaji wa miradi ya BOOST yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 419.
Serikali kupitia mradi wa uboreshaji elimu ya awali na msingi (BOOST), imeipatia Mji Mbinga kiasi hicho cha fedha kwaajili ya ujenzi wa madarasa 15 na matundu 30 ya vyoo katika shule za msingi Beruma, Masumuni, Nazareth, Changarawe na Luhangai.
Afisa Elimu Takwimu, Idara ya Elimu ya Awali na Msingi, Halmashauri ya Mji Mbinga, amesema kuwa nguvu za wananchi zitaokoa fedha ambazo zingetumika kuajiri vibarua.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetupatia pesa, shukrani yetu ni kwa sisi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi,” alisema Bw. Mwihava.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.