Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wahimizwa kumeza Kinga Tiba za Usubi ili kutomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele ya kichocho, matende na mabusha, minyoo pamoja na usubi.
Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa magonjwa yasiopewa kipaumbele kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Washa Washa wakati wa ufunguzi wa zoezi la umezaji Kinga Tiba za Usubi tarehe 17 Agosti 2023 uliofanyika katika Kijiji cha Burma.
Amesema kuwa kila mwananchi mwenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea isipokuwa mjamzito pamoja na mgonjwa mahututi anatakiwa kumeze dawa hizo ili kuwa salama.
Amebainisha kuwa bado jamii haina elimu ya kutosha juu ya faida za Kinga Tiba hizo na baadhi ya wanafamilia wamekuwa wakiwafukuza watoa huduma wanaopita katika Kaya zao kwa lengo la kuwapatia dawa hizo muhimu kwa afya zao.
" Tukiongelea ugonjwa wa Usubi tuna watu wetu ambao wanao lakini bado hatuna elimu ya kutosha, mfano dalili za usubi ni pamoja na kuwasha mwili, kua na uoni hafifu na kuwa na mabaka mabaka kwenye ngozi zetu" Amebainisha Washa Washa
Amebainisha kuwa kwa mwaka 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeweza kuwafikia wanajamii na kuwapatia kinga tiba ya usubi kwa asilimia 84% ikiwa walengwa walikuwa 283,531 na walifikiwa ni 237,249.
Washa Washa amebainisha madhara yatokanayo na ugonjwa wa usubi ni kusababisha upofu pamoja na kupunguza nguvu kazi katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.