Katika juhudi za kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na utawala bora, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizindua jengo jipya la utawala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mnamo tarehe 25 Septemba 2024.
Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya miaka minne ya uongozi wake.
Jengo hili limekuwa mwarobaini wa changamoto zilizowakumba watumishi wa Halmashauri hiyo, ambao awali walilazimika kufanya kazi katika majengo tofauti.
Hali hiyo ilisababisha ugumu wa utekelezaji wa majukumu yao na kuwapa wananchi adha na usumbufu walipohitaji huduma za wataalamu wa Halmashauri.
Kwa sasa, jengo hili limeleta urahisi na ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa Mbinga.
Watumishi wanafanya kazi katika mazingira bora zaidi, hali inayochochea utendaji kazi wenye tija na kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Uzinduzi wa jengo hili ni sehemu ya dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha mifumo ya kiutawala na kuboresha huduma za umma. Kupitia miradi kama hii, Rais Dkt. Samia ameendelea kuthibitisha nia yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa vitendo.
Kwa heshima na shukrani, wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wametoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuboresha maisha ya Watanzania.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.