Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Mheshimiwa Hussein Bashe ameyataja maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuongeza mtandao usambazaji mbolea ya ruzuku vijijini ili kuondoa kero ya wakulima kufuata mbolea mbali.
Mheshimiwa Bashe ametoa maelekezo hayo wakati anazungumza na baadhi ya wakulima wa kijiji cha Muhukuru Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ambapo pia amekagua ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji katika kijiji hicho.
Waziri Bashe yupo mkoani Ruvuma katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo anatembelea Wilaya za Songea na Namtumbo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.