MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Mariam Nyoka,ametoa msaada wa pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni 2.5 kwa familia yenye mapacha watatu inayoishi kijiji cha Mkapunda wilayani Tunduru ili iwaingizie kipato kitakachosaidia kwenye malezi ya watoto wao.
Baba wa watoto hao Hamis Shaibu alisema,baada ya kujaliwa kupata watoto mapacha wanne alilazimika kumuomba Mbunge pikipiki ili iwasaidie kulea watoto kwa kubeba abiria kutokana na changamoto ya maisha waliyonayo.
Alisema hana kazi wala shughuli yoyote ya kumuingizia kipato,jambo ambalo lingeweza kumsumbua katika malezi ya watoto wake hasa ikizingatiwa kwamba yeye ndiyo kichwa cha familia licha ya mama wa watoto hao Judith Sichawe ni Mwalimu wa shule ya msingi.
Amemshukuru Mbunge kutokana na msaada huo,na kuhaidi kutumia pikipiki hiyo kufanyia biashara itakayowaingizia kipato ambacho kitakwenda kupunguza ukali na ugumu wa maisha kwenye safari ya malezi kwa watoto wao.
Aidha,amewaomba wasamaria wengine kuendelea kuwasaidia katika malezi na matunzo ya vijana wao kwa kutoa walichanacho kwa sababu watoto hao bado wana uhitaji wa vitu vingi.
Naye mama wa watoto Judith Sichawe alisema,alifanikiwa kujifungua mapacha wanne hata hivyo kwa bahati mbaya mtoto mmoja amefariki Dunia tangu mwezi Septemba mwaka jana na sasa wamebaki watatu wenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili
Mbunge wa viti maalum Mariam Nyoka alisema,amelazimika kutoa msaada huo kwa kuwa anatambua ugumu wa kulea na kutunza watoto mapacha kwa wakati mmoja na changamoto ya kimaisha inayoikabili familia hiyo.
Alisema,hiyo ni mara ya pili kuitembelea na kutoa msaada kwa familia hiyo yenye jukumu kubwa la kulea watoto wao hadi pale watakapokuwa watu wazima na kuanza kujitegemea.
Kwa mujibu wa Nyoka,kulea watoto mapacha watatu ni kazi ngumu inayohitaji kipato kikubwa,na yeye kama sehemu ya jamii ameona ni vyema kuisaidia familia hiyo pikipiki ambayo itakuwa chanzo kikubwa cha kuwaingizia kipato.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.