Mbunge wa Jimbo la Madaba, wilayani Songea mkoani Ruvuma Dkt Joseph Mhagama ameyataja mafanikio makubwa katika sekta ya afya kwa kujengwa kwa Kituo cha Afya katika Kata ya Mtyangimbole.
Amesema kituo hicho kinatoa huduma za afya zinazofanana na hospitali ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya.
Awali, wakazi wa eneo hilo walilazimika kutibiwa katika Zahanati ya Misheni.
Akiwa katika ziara ya kikazi ya kueleza utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka minne na kupokea changamoto za wananchi, Dkt Mhagama amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaodai serikali haijafanya chochote.
Ameeleza kuwa tangu nchi ipate uhuru, eneo hilo halikuwahi kuwa na Kituo cha Afya, hivyo ameishukuru Serikali kwa kufanikisha ujenzi huo.
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.