Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Vitta Rashid Kawawa amekabidhi mifuko ya simenti 40 na madawati 30 katika shule ya msingi Upendo .
Akikabidhi mifuko hiyo pamoja na madawati Kawawa alisema anatimiza ahadi yake aliyohaidi katika ziara yake ya tarehe 16.9.2023 alipotembelea Kijiji Cha Mputa na wananchi kumwomba msaada wa kuisaidia shule ya msingi upendo
Aidha Kawawa aliwashukuru wananchi wa Kijiji Cha Mputa Kwa ushirikiano wao wa kujenga shule ya msingi Upendo lakini akadai Ofisi ya Mbunge itahakikisha shule hiyo inapata fedha kama shule zingine .
Hata hivyo Kawawa alimwagiza Afisa elimu vifaa na takwimu aliyemwakilisha afisa elimu msingi katika makabidhiano hayo kuwa ofisi ya elimu msingi inatakiwa kutenga bajeti ya kujenga madarasa ,Nyumba za walimu na vyoo Kwa ajili ya shule hiyo
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Lulu Mapunda alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Kwa kuisaidia shule hiyo madawati 30 na mifuko ya simenti mifuko 40 Ili kuisaidia shule hiyo kuboresha miundombinu yake.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.