Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, Leo ametembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa. Aidha ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi huu na amemtaka Mkandarasi anayejenga Suma JKT kuongeza kasi ya Ujenzi na kukamilisha ujenzi kwa wakati kwa kuwa, Ofisi inahitajika sana ili Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wafanye kazi katika mazingira mazuri.Pichani (Katikati)Ni Mbunge huyo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama (kushoto) na Afisa Mipango Wilaya ya Nyasa Bw. Jabir Chilumba (kulia).
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.