Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, limeiomba Serikali kuwasaka na kuwadhibiti waganga wote wa tiba asili, ambao wanawanywesha akina mama wajawazito dawa za kuongeza uchungu wa kujifungua, ili kuzuia vifo vya akina mama wajawazito ambavyo vimekua vikitokea kabla hawajafika hospitali kutokana na kunywa dawa hizo nyingi kupita kiasi.
Akiongea katika baraza hilo, Mbunge wa Jimbo la Nyasa. Mhandisi Stella Manyanya amewataka pia wanawake wilayani humo, kuacha tabia ya kujifungulia nyumbani na kwamba Serikali imeshajenga zahanati na vituo vingi vya afya kwa lengo la kuhakikisha maisha ya mama na mtoto yanakua salama.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.