Muonekano wa Meli ya MV Mbeya II katika ziwa Nyasa, yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo .Mbunge wa Jimbo la Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya anasema meli hiyo ndiyo ukombozi wa wakazi wa Mwambao mwa ziwa Nyasa kwa sababu italeta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wake wa Jimbo la Nyasa na Mkoa mzima wa Ruvuma.
Amesema meli hiyo ya abiria itaondoa kabisa adha ya abiria ambao wamekuwa wakipata tabu sana kusafiri tangu meli ndogo ya MV Songea iliposimama kutoa huduma katika ziwa Nyasa kutokana na kutokuwa katika hali nzuri.
Kwa mujibu wa Shirika la Bandari Tanzania,MV. Mbeya II itatoa huduma katika bandari zote za mwambao wa ziwa Nyasa ikiwa ni pamoja na nchi jirani za Malawi na Msumbiji, hivyo kurahisisha shughuli za wafanyabiashara mbalimbali wanaosafiri na kusafirisha mizigo yao kwenda na kutoka maeneo mbalimbali ya mwambao wa ziwa Nyasa.
Meli ya MV Mbeya II inaudwa baada ya meli ya mwanzo ya MV Mbeya I kuzama mwaka 1975 eneo la Makonde wakati ilipokuwa ikifanya safari zake za kawaida katika ziwa hilo.
Ujenzi wa meli hii ni muendelezo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutatua changamoto ya vyombo vya usafiri wa majini, baada kukamilisha ujenzi wa meli mbili za awali MV Ruvuma na MV Njombe kwa ajili ya kusafirisha shehena ambapo tayari zimeanza kutoa ajira za moja kwa moja kwa wakazi wanaozungukwa na bandari hizo hususani mikoa ya Ruvuma,Njombe na Mbeya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.