NUNDASUCHUS SONGEAENSIS ni mnyama ADIMU Duniani aliyewahi kuishi katika bonde la mto Ruhuhu unaotengatisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma upande wa Manda, maeneo ya Ngingama kuelekea Lituhi. Ni kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Allan (PhD) wa Uingereza. Utafiti aliofanya mwaka 1932.
Ni mnyama ambaye amekuwepo kabla ya uwepo wa Dinosaur na umaarufu wake. Mabaki ya vizazi vya mnyana huyo (reptile) ni mamba wa sasa. Mnyama huyo alipewa jina kutokana na sifa za mabaki ya vizazi vyake kuwa ni viumbe wabishi, basi wenyeji mtu au kitu chenye ubishi hukiita "nunda".
Nchini Ugiriki kwa mujibu wa Hekaya za Kigiriki (Greek Mythologies) zamani kukikuwa na mungu aliyetwa "suchus" ambaye alikuwa mungu wa mtoni. Ni zama za uwepo wa imani za miungu wengi. Basi Dr. Allan alimwita mnyama huyo jina la kwanza ni Nundasuchus. Jina la pili ni mahali alikopatikana, Songea. Zamani hizo Songea ilijumuisha eneo kubwa hadi Manda. Basi mnyama huyo aliitwa Nundasuchus Songeaensis (nyongeza ya kiambishi -ensis cha Kigiriki).
Pamoja naye waliojulikana baada ya utafiti kuna mnyama NYASASAURUS PARINGTONI (hayupo pichani) na MANDASUCHUS TANYAUCHEN (picha ya juu). Ni majina ya Kiswahili yaliyochanganywa na Kigiriki. Bonde la mto Ruhuhu historia yake ni ndefu na ni mto wenye mamba wengi jamii ya Nundasuchus.
Makala Imeandikwa na Marcus Mpangala,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.